UZI
Unawezaje kutumia IMEI namba kufatilia(track) simu yako iliyopotea?
Twende sawa utanielewa tu bila shaka
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Takwimu za sasa zinaonyesha kwamba milioni 70 ya simu zinapotea kila mwaka.
Utajiuliza je wamejuaje?usiwe na shaka twende sawa utanielewa.

Simu yako bila kuwa na laini,GPS location au upatikanaji wa mtandao (Internet access)kwa muda mrefu inahesabika kuwa imeepotea au kuibiwa.
IMEI(Internation Mobile Equipment Identity) ni tarakimu 15 ambazo zimethibitishwa na Mamlaka ya Simu za mkononi duniani(GSMA) na kuwa utambulisho wa kila simu.
nadhani tunaelewana twende sawa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Mara nyingi simu hutumia mtandao kuweza kupiga,kupokea au kutuma ujumbe hivyo IMEI ya simu yako hutumwa moja kwa moja kwa watoa huduma wa kimtandao au maaskari (sio maasikari wetu uchwara wa sisiemu๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€)wenye database ambazo hutunza IMEI za simu iliyotumika.
Twende sawa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Hivyo mtumiaji anaweza akaripoti kituo cha polisi na simu ikafungiwa au kuifatilia simu ilipo baada ya kuibiwa au kupotea.
Baadhi ya watu hutumia Bluetooth tracer GPS locator kuweza kuipata simu iliyokaribu walakini aina ya upatikanaji wa simu yako kwa
kutumia Bluetooth tracer GPS locator ina vizuizi vya umbali usiozidi mita 10 lakini simu yako inapochukuliwa au kuibiwa zaidi ya umbali wa mita 10 unaweza kutumia namba ya IMEI na anti theft tracker ili kujua simu yako iko wapi na kuifanya isiwe na kazi yoyote kwa aliyeiiba au
kuichukua.
Nawezaje kupata namba IMEI ya simu yangu?Ni rahisi sana.
Bila shaka tunaelewana twende sawa ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Njia ya haraka zaidi ni kubonyeza
*#06#
Njia nyingine ya kupata IMEI ni kwenda moja kwa moja kwenye setting na ubofye "About Phone" utaipata kama inavyoonekana hapa chini
Mara nyingi namba ya IMEI inaweza ikawa nyuma ya simu unapoigeuza na kutoa betri la simu, Pindi tu simu unapoipoteza au kuibiwa usiwe na shaka kuhusu IMEI kumbuka unapackage ya boksi ulilonunulia simu ukiangalia kwa umakini lebo ya IMEI namba zako za simu inakuwepo pia.
Unawezaje kuipata simu yako iliyopotea kwa urahisi zaidi.
Hakikisha una simu nyingine ambayo ina Anti-theft app au IMEI tracker app. Apps zinapatika google play store.Hakikisha simu yako ina Android version kuanzia 4.4 au zaidi ili kuweza kuendesha hii App.
Baada ya kuinstall app ruhusu hiyo app kuweza kujiendesha ikiwa na mifumo mingine kama vile camera,contacts n.k kama unavyofanya kwenye application zingine
Weka namba ya IMEI ya simu yako iliyopotea na uanze kuifatilia.Hivyo kuna dirisha dogo litatokea ambalo linaonyesha simu yako ilipo kwa maana ya jina la sehemu simu yako ilipo.
Hivyo IMEI haionyeshi tu kwamba simu yako ilipo vile vile inaweza ikakusaidia kulinda simu yako kwa kutengeneza namba za pini.Unaweza ukaifanya chochote simu yako iliyoibiwa kwa kutuma codes au pin na kuifanya simu yako ikaanza kupiga alarm au kukutumia jina la sehemu simu yako
ilipo. Kama simu yako unaipenda sana hifadhi IMEI zake usisahau pia kuna watu ni wajuzi wa kubadilisha IMEI.Kumbuka hii ni kwa wateja wa simu za android tu. Stay safe wazee โœŒ
You can follow @ChumaPua.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword โ€œunrollโ€ to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: