Ufahamu wangu kuhusu hali ya sasa ya mziki na yatakayojiri baada ya COVID-19. Ufahamu huu ni wa biashara.

Tuelewane kwamba kwa wasani Tanzania, mapato makubwa yanatokana na
1. Youtube
2. Live performance (nje ya nchi zinalipa zaidi),
3. Endorsements &
4. Mitandao ya miziki.
Vyanzo vyote vya mapato vimevurugwa (disrupted) na COVID-19

1. Youtube - Matangazo duniani kote kwa mtandao huu yameshuka, hivyo mapato yatashuka pia kwa wasanii

2. Live Performance - Hazitowezekana kwa sasa mpaka chanjo itakapopatikana ndani ya miaka miwili
3. Endorsements - Kwasababu hali ya biashara duniani ni mbaya na watu hawana pesa sasa hivi ni ngumu kuona makampuni yana-push matangazo

4. Mitandao ya miziki - Hiki bado kinabaki chanzo kizuri kipndi hichi lakini sio chenye faida sana.
Imani potofu ni kwamba wasanii wanamini COVID-19 itakwisha miezi mitatu ijayo na dunia na bishara itarudi kama ilivyokuwa mwanzo. Kitu ambacho sio kweli.
Nchi za Ulaya na Marekani wanapotegemea kwenda kufanya show ili kulipwa hela nzuri, huko hali zao za kiuchumi ni mbaya.
Miji mikubwa kama Los Angeles tayari imefuta shuhuli zote za mikusanyiko mpaka 2021. Na tunategemea chanjo kupatikana ndani ya miezi 18 inayokuja ili kuweza kuanza kuruhusu shughuli za mikusanyiko

Swala la msingi linakuja, je hii miaka miwili unaishije?
Ushauri:
1. Cash. Pesa uliyonayo itumie kwa uangalifu mkubwa sana. Kuna uwezekano wa kumaliza hii covid-19 na madeni na ukashindwa kurudisha. Usifanye uwekezaji wowote kwa sasa hivi.

2. Record. Huu ndio muda mzuri wa kukaa studio na kutengeneza nyimbo za kutosha.
3. Connect. Tumia Mitandao ya kijamii kuconnect na mashabiki wako na si kuwatumia matangazo na ma challenge. Nimependa sana idea ya @JideJaydee ya Quarantine Gigs

4. Content. Tengeneza maudhui ya Video na Sauti kuweza kutumika katika mitandao kama youtube, boomplay, audiomack ->
Kwasababu watu hawana sehemu za starehe kwenda, basi watatumia mitandao hii kupata burudani. Hakikisha wakiiingia humo ndani wanakuta kazi zako. Ili haya mambo yakiisha wawe wame "connect" na wewe.

Fanya kama vile hii hali ya sasa itadumu kwa muda wa miaka miwili.
Mwisho, jua kabisa hii janga limevuruga dunia nzima ya burudani na baada ya hii hali kwisha mambo yatakuwa tofauti milele. Ni kujidanganya kwamba mambo yatarudi kama zamani.
You can follow @MikieMushi.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: