AN OPEN LETTER 💌 TO MY FUTURE SON.

Dear son,
Najua bado upo umening'inia katikati ya mapaja yangu na ndani ya nyonga ya mama yako mtarajiwa. Sijui ntakuleta lini duniani lakini natamani siku utakapokuja basi uikute hii barua yako.
T H R E A D 👇
Dear son, natamani nikupate kama mtoto wangu wa kwanza kwenye familia ili ukomavu wako kama mwanaume uwe nuru kwa wadogo zako.
Natamani pia uwe wa pili kuzaliwa baada ya dada yako ili kutokana na yeye kuwa mkubwa wako basi utajifunza kumheshimu kila mwanamke utakae kutana naye
Mpendwa kijana wangu, changamoto ni nyingi sana hapa duniani. Umri wa kukuleta unawezakua umefika lakini wakati wa kukuleta ukawa bado haujafika.

Tizama siwezi kuruhusu kukuleta mapema ndani ya dunia hii chungu kwa mtu ambae bado maisha yake hayana uelekeo endelea kusubiri
Dear son, wanawake wengi wanasifa ya kuwa mke wangu lakini sio kila mwanamke anasifa ya kuwa mama yako.
Nataka nikutafutie mama ambae hata wakisimama wanawake 1000 ukaambiwa uchague yupi anafaa kuwa mama yako bado utaendelea kumchagua yuleyule mama yako
Simaanishi baba yako nipo na standards sana au levels NO. Nachomaanisha ni kwamba sio kila anaevaa sketi anafaa kuibeba mimba yako.
Apatikane yule mama yako ambae hata akipita pale sebuleni ukiwa umekaa unatikisa kichwa like
" Yes baba alivaa miwani wakati anachagua"😄
Dear son, baba yako sikupanda basi la njano lakini we hata ukitaka bus la blue au kijani ntahakikisha unapanda Ukapate maarifa.

Lakini hata ikishindikana, fagio na kidumu vitahusika maana hata huku ni kuzuri zile changamoto zitakujenga sababu "school bus" watakupa maarifa
Lakini "fagio na kidumu" watakupa busara ya kupambana na changamoto.
Dear son, sitokulazimisha kuwa wa kwanza darasani we usifeli wala usiwe zile namba mbaya maana hata aliyekua anakuwa wa kwanza kipindi kile nasoma saivi ndo ananipiga mizinga ya hela 😂
Baba yako ntakua mwalimu wako wa kwanza,japo simaanishi ntakufundisha Algebra wala hesabu za kutafuta Umri NO.
Ntajitahidi nkufundishe namna ya kuishi na watu kwa sababu 80% ya maisha yako hautoishi na ndugu zako bali ni Walimwengu huko Masomoni
Dear son,
Nitakua mchungaji wako wa kwanza pale nyumbani. Nitakufundisha jinsi ninavyoitafsiri dini na jinsi navyomjua Mungu. Nitakuelekeza nafasi ya upambanaji na uhusiano kati ya hustle na Mungu.
Sitoruhusu upotee na imani za "pokea gari " mara " pokea nyumba"
You'll die poor
Dear son, nitakuelekeza maisha yanataka nini. Nitakuonesha kurasa zangu nzuri za maisha yangu ili ujifunze na kufanya zaidi
Nitakuonesha baadhi ya kurasa zangu mbaya za kitabu changu cha maisha ili usipite njia mbaya nlizopita mimi maana kuna wakati hizo kurasa natamani nichane😂
Utakua mshikaji wangu, utakua rafiki yangu. Nitaruhusu uoneshe hisia zako kama binadamu, nikipatia nipongeze nikizingua onesha kabisa nimezingua,chukia panapobidi (lakini itifaki izingatiwe)😀
Mama yako ni mke wangu. Jua namna yakuishi nae kama mama yako na kama mke wa baba yako
Dear son, nakuandalia maisha yako yawe vizuri ili siku moja upige picha ukiwa chuo na ukiwa nyumbani pia sio tuu unapiga picha ukiwa chuo tuu😂
Btw urithi wangu hautakua elimu tu,lazima nikupe kianzio usipate shida kama mimi.
So dear son, sitokuforce jambo. I'll never force your "Right" to be " wrong" or your "Yes" to be " No". Japo ntacheza nafasi yangu kama baba.
Ntakuwa muwazi kuhusu mahusiano, ntakuelekeza mwanamke anataka nin coz love ni hustle na ukitegemea "upepo wa kisulisuli " utakufa single
Kuna time ntakua daddy,kuna time ntakua baba, saa zingine mshua,saa zingine dingi so ntakua chochote unachotaka kwa wakati husika.
Regard your future father @Vet_doctor87
#End
#MyMindSpeak
#NohTalk ☕️
You can follow @Vet_doctor87.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: