IN MY HUMBLE OPINION. Part 2️⃣

Note:Hii ni ndefi kidogo. Kama wewe mvivu wa kusoma kaa mbali.

Part 1 nilitoa MAONI/MTAZAMO wangu nikajaribu kuelezea kwanini "TOTAL LOCKDOWN" itakuwa sio uamuzi wa busara/sahihi. Part 2 Nitajaribu kuelezea Mbadala (alternative) ya nini kifanyike.
1:FUNGA MIPAKA

Hii itasaidia sana kuzuia TZ kutopokea maambukizi ya Virusi Vya CORONA kutoka nchi jirani na pia TZ kutopeleka maambukizi kwenye nchi hizo,mfano mzuri MTZ aliekwenda kenya na kukutwa na CORONA. Nafikiria ni uamuzi sahihi na wa busara kuchukua hatua hii MUHIMU⬇
itaakayowalinda WANANCHI WETU KWANZA. Hoja ya kuwa tusipofunga mipaka yetu "TUTAWAUWA" nchi hizo ni dhaifu sana hasa ukizingatia imetoka kwa kiongizi mkuu wa nchi. Jiulize wao wanavyofunga mipaka yao je wanataka kujiuwa? je wanataka kutuuwa sisi?

TUFIKIRIE WANANCHI WETU KWANZA
2:ZUIA SAFARI ZA NDANI

Hivi majuzi kulikuwa na taarifa watu waliotoka Tanga kwenda Zanzibar na kukutwa na maambukizi. Hii inaonyesha imefika mda sasa wa kuzuia watu kusafiri kutoka wilaya/mkoa kwenda wilaya/mkoa mwingine ili kudhibiti maambukizi kusambaa maeneo mengine kwa kasi.
Kama mtu atakuwa na ulazima wa kusafiri kutoa wilaya/mkoa kwenda wilaya/mkoa mwingine basi awekwe karantini siku14, apimwe ndipo aruhusiwe kusafiri. Hii itasaidia kuongeza idadi ya watu waliopimwa na pia itadhibiti mambukizi kusambaa hovyo na kufanya ufuatiliaji wake kuwa mgumu.
3:PIGA MARUFUKU MIKUSANYUKO ISIYOKUWA YA LAZIMA.

Ili kuepusha mikusanyiko ya watu itakayopelekea kusambaa kwa haraka na kwa watu wengi, serikali inabidi ipige marufuku sehemu/shughuli zenye mikusanyiko isiyokuwa ya lazima hadi pale hali itakapokuwa shwari. Marufuku hiyo iguse⬇
A:SEHEMU/SHUGHULI ZA STAREHE NA MISIBA

Itakuwa ni busara sana kuzuia sherehe zote za harusi na pia kufunga kumbi zote za starehe (bar, Night clubs) sehemu za mazoezi (GYMS) michezo ambayo bado inaendelea mitaani kama Mipira,Bao,Pool table hadi hapo hali itakapokuwa shwari.
Itakuwa ni ujinga wa kihistoria kama mtoto aliyekuwa boarding kigoma akatolewa na kurudishwa nyumbani dar es salam ili asipatwe na maambukizi ya corona halafu aje kupata maambukizi kwa mzazi wake anayekwenda bar, kwenye masherehe ya harusi na sehemu/shughuli zingine za starehe.
Marufuku hii pia iguse Misiba ambapo imekuwa ni desturi kuwa na wahudhuriaji wengi na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa watu. Hivi sasa wahudhuriaji kwenye msiba wawe ni ndugu jamaa na marafiki wa karibu tu na piwa kuwe na kikomo kwenye idadi ya wahudhuriaji kwenye msiba.
B:NYUMBA ZA IBADA (MAKANISA, MISIKITI, MAHEKALU nk)

Ili kuepuka kusambaa zaidi kwa maambukizi itakuwa ni busara kupiga marufuku hadi hali itakapokuwa shwari, lengo kuepusha mikusanyiko, na Viongozi wa dini wakatafuta njia mbadala ya kuendesha ibada eg Redio/TV na social media
Biblia inasema "watu wangu WANAANGAMIZWA kwa kukosa MAARIFA kwa kuwa wewe UMEYAKATAA MAARIFA mimi nami NITAKUKATAA" wewe.

Dhana (=UPOTOSHAJI) kuwa ukienda kwenye nyumba ya ibada hautapata maambukizi ni KUYAKATAA MAARIFA na ni ujinga uliopitiliza Unaohatarisha maisha ya wengi.
Africans know French better than the French. Msemo huu unaongelea hali halisi iliyopo Afrika/TZ. Wakati waliotuletea dini huko Jerusalem,Vatican,Mecca wamesitisha ibada kwa mda kudhibiti maambukizi kusambaa sisi TUNAKAIDI kama vile maambukizi haya yanajali upo Msikitini/Kanisani.
Kwa vile lengo ni kupunguza mikusanyiko/msongamano wa watu Marufuku hii iguse pale panapouzwa chakula na vinjwaji kama mahoteli/migahawa/vioski mama ntilie (nk) na watu wasiruhusiwe kuketi sehemu hizi na badala yake watoe huduma kwa njia ya kuuza kwa mfumo wa delivery/take away.
C:MASOKO

Ili kuepuka misongamano kwenye masoko serikali iruhusu maeneo ya wazi (mfano viwanja vya mpira) kutumika kwa muda hadi hapo hali itakapokuwa shwari. Hii itafanya kuwe na masoko mengi na yalio karibuu na watu na kuepusha misongamano ya kusafiri kwenda Masoko ya mbali.
Shughuli zingine za kuuza na kununua bidhaa mbalimbali zinaweza zikafanyika kwenye mitandao mbali mbali chini ya uangalizi wa mamlaka husika hivo kuepusha misongamano/mikusanyiko ya watu katika sehemu mbalimbali (mfano kariakoo).
4:SERIKALI IJE NA MIPANGO MKAKATI YA KUPUNGUZA MAKALI KWA WANANCHI

Serikali ikishirikiana na mifuko ya jamii kwa wafanyakazi na wa umma, waje na mipango ya kupunguza makali kwa wananchi. Mipango hiyo inaweza ikawa kwenye kusaidia kupunguza bei ya huduma za umeme na maji ama ⬇
KUFUTA KABISA gharama hizo kwa wale walioathiriwa na janga hili,ama kama motisha kwa wale watakaobaki majumbani. Mipango hiyo pia ielekee kupunguza kodi/ushuru (pengine kufuta kabisa) kwenye biashara ndogo ndogo zitakazokumbwa na hasara kubwa kutokana na janga hili la corona.
Mipango hii pia inaweza kuwapunguzia kiasi cha kodi makampuni yatakayokubali kufunga ofisi/shughuli zao na kuwaruhusu wafanyakazi wao kufanya kazi wakiwa majumbani kwao ama kufunga kabisa ofisi/shughuli zao huku wakiendelea kuwalipa wafanyakazi hao mshahara wao kwa kiwango flani
Serikali pia itumie chakula kilichopo katika ghala la taifa kukisambaza kwa wale masikini,yatima pamoja na wale waliopo kwenye mazingira magumu na wasiojiweza, pia fedha zilizotengewa kwenye mfuko wa maafa (kama hakuna zitengwe) ili zielekezwe katika kusaidia kupambana na corona.
Mwisho kabisa serikali itumie makampuni ya simu kuwafiki wananchi na kuwafikishia taarifa muhimu na pia kutoa elimu kwa njia ya sms juu ya dalili na jinsi ya kujikinga na maambukizi na kuendelea kuwasisitiza kuepukana na Msongamano/mikusanyiko .

Na muhimu kuliko zote ni vipimo.
Serikali ihakikishe injitahidi sana kupima watu wengi iwezekano ili kujua idadi na pia kuwa isolate wagonjwa ili wasiambukize wengine na piwa wanakuwa wazi katika utoaji taarifa.

NOTE:Haya ni MAONI/MTAZAMO WANGU
#COVID
#StayAtHome
#coronavirus
#Nawamikono

Stay safe
+ Part 2 @MariaSTsehai
You can follow @frankeli007.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: