Jana tukatuma press release juu ya hizi CRB. Wasee wakadunda ndani ya inbox yangu: Fadhela ebu kuja ufafanuate hizi stori. Naelewa kingoso lakini staki vitu zinipite. Hii maneno ya CRB mlikuwa mnasema nini?

Nikafikiria, nikaamua the best thing ni?

Ka-uzi, wadau...

1/14
Saa hii maze vitu zimekuwa ngori. Corona noma. Job inakaa ni kama itakatika, na hustle pia inakaa noma. Uko na m-junior hapo anadai maziwa na malenge. Yeye hajui corona, anajua wewe ni budake au mathake na contract yako na Sir God imesema ushughulikie familia.

2/14
Unajiambia lazima utafute unga. Unafungua ka-biz au unaendeleza. Hata unajiambia innovation is the mother of creativity. Biz ya kinyozi hadi unaambia watu watulie - utawanyolea home kwao. Hata unasatinize machine zako zote na unajitakasa vi-proper.

3/14
Au nduthi badala ya kubeba abiria utafanya ma-delivery. Unatuma ma-WhatsApp kwa kerende unawashow - nitumieni shopping list mimi nita-make sure nakuletea vitu haraka na kwa usafi, na bei yangu ni poa. Unajiambia at least Sir God amekucheki na good health, na unajichunga.

4/14
Tuseme hata kuna vile biz imechacha hadi unataka kununua machine ingine ya kinyozi upatie boy wako job. Au hiyo nduthi ikatike chain na huna ganji ya kufanya repair. Ama wewe una janta ya kuwa tailor na unaona ununue cherahani extra juu job imeongezeka.

5/14
Ama ikuwe kuna job fulani umeitiwa. Unaambiwa uje na cert of good conduct unasema hiyo ni sawa, mimi sijawahi kuwa dingo. Alafu unaambiwa pia CRB cert. Unaanza ku-sweat. Hii ndio job ya kwanza kutoka chuo utapata wapi ganji ya kulipia hiyo cert? Si uanze job kwanza?

6/14
Wadau, hizo zote ndio scenario tulikuwa tunacheki. Kuna wadhii wakijaribu kukopa doo ya kujimudu na kuongeza hustle wanaambiwa wako ati blacklisted. Juu kuna ka-twenty bob fulani ati hujawahi lipa. Ukijiuliza hata huoni ni nani huyo ulidinda na rwabe yake, lakini blacklist.

7/14
Unasikia ni kama mtu amekuweka pingu. Vile CBK wanasema ni ati hakuna kuwekwa blacklist unless madeni zako zimepita thao moja. Sio ati uzoee kuhepa na ganji ya watu, lakini maisha haifai kusimama juu ya doo kidogo. So, ikiwa deni haijapita kavu moja, hakuna blacklist.

8/14
Pia hii story ya kuitishwa CRB clearance. Ukitaka hiyo certificate ya first, utaitisha na watakupatia bila kukulipisha. Ndio isiwe hizi ma-opportunity zinakupita juu hauna doo ya kulipia hiyo cert moja.

9/14
Wadhii wengi wako kwa sacco. Unajua wewe hukopa doo na unalipa vizuri bila makasiriko, hii sasa itakuongezea marks kwa hiyo report yako ya CRB.

10/14
Kuna vile pia hawa wasee wa kukukopea doo kwa simu wana-smile alafu ukichelewa na siku moja unasikia hata hedi wenu na pastor huko ocha amepigiwa simu ndio wakuaibishe. CBK imesema hiyo ni ufala. Hiyo ni kuchukua membership kwa kamati ya roho chafu na haifai.

11/14
Ya mwisho ni gava imeona hii corona ni nuks tupu. So last week wakapitisha ati for now, hautaanikwa juu umeshindwa kulipa doo umekopa. Wanakupatia space ujipange. Hustle ikiiva na corona iishe at least hautakuwa umengojewa pale nje na wale wasee wa ile video ya coffin.

12/14
Hiyo yote ni ya kusaidia wadhii, especially kama uko na bizna ndogo, na especially kama wewe ni m-yout, uwe na space ya kujipanga na kujishikilia hadi hii noma itupite. Tunacheki vile maze hii life inaweza kutukoroga, lakini tuone vile tutasurvive.

13/14
Lakini please msichukulie hizi stori alafu mjibebe malenge. Ati uanze ile tabia wengine wamezoea ya kukopa doo alafu unaanza kuwekelea bet. Juu hata sioni bet iko wapi na hakunanga ball siku hizi. Jibebe kama mtu wa nguvu, mtu wa heshima. Osha mkono. Kaa mbali na watu.

14/14
You can follow @wgkantai.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: