HEBU LEO MJUE VIZURI HUYU MTU WA MIUJIZA AITWAE NG'WANAMALUNDI SHUJAA WA WAKISUKUMA ALIYEWATESA WAKOLONI.

Mwanamalundi ni jina ambalo lilikuwa maarufu sana karne ya 18 na 19 (enzi za mkoloni) maeneo ya kanda ya ziwa; hususani Mwanza na Shinyanga.
MWANAMALUNDI NI NANI HASA?

Mwanamalundi ni jina la mtu wa miujiza kutoka kabila la Wasukuma. Matamshi sahihi ya jina hili Ni "Ng'wanamalundi" na sio "Mwanamalundi" kama ambavyo wengi hutamka.
Mwanamalundi alizaliwa kijiji cha Ng'wakwibilinga, wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza mwaka 1892. Baba yake aliitwa Bugomola na mama yake aliitwa Ngolo. Wazazi hawa wawili hawakujaaliwa kupata watoto kwa muda mrefu sana.
Ni nyakati ambazo hakukuwa na makanisa ya maombezi kama ilivyo leo hii, misikiti ya kuomba dua wala hospitali. Waganga ndio watu pekee waliotatua matatizo mbalimbali ya jamii zao.

Mzee Bugomola na mke wake Ngolo wakaamua kwenda kwa mganga ili watatue tatizo lao
Mganga akawatengenezea dawa kisha akawaambia kuwa Ngolo (mama/mke) atashika mimba na atazaa mtoto wa kiume ambae atakuja kuwa mashuhuri siku za hapo baadae lakini kwa bahati mbaya Bugomola (baba/mume) hatoweza kumuona mtoto huyo; yaani Bugomola atafariki kabla mtoto hajazaliwa.
Baada ya wiki kadhaa Ngolo alishika mimba. Mimba ilipotimiza miezi mitatu tu, Bwana Bugomola aliaga dunia bila hata kuugua. Ngolo ambae alikuwa mjane wakati huo aliilea mimba hiyo hadi ilipofikisha miezi 9.
Unaambiwa Siku moja kabla Ngolo hajajifungua mtoto, wingu kubwa lilitanda angani. Mvua kubwa na yenye radi kali ikaanza kunyesha. Mtoto aliyekuwa tumboni akaruka mruko usio wa kawaida na kisha ikaskika sauti ya kitoto kutoka tumboni ikisema, "máyo nibyalage, yaani mama nizae!"
Ilikuwa ni miaka ya 189Os kiume mwenye maajabu tangu akiwa tumboni mwake. Mtoto huyo akaitwa Igulu, yaani Mbingu.

Igulu (Mwanamalundi)alizaliwa akiwa na afya njema,  isipokuwa alikuwa na miguu mimbamba na nyao za miguu yake ikiwa ni mikubwa isiyo kawaida.Huyo ndo (Mwanamalundi).
Alikuwa ni kijana mwenye aibu sana aliyependa sana kucheza na marafiki,  watoto wenzake walimpenda sana na kupenda kuzurura kwa pamoja..kitu ambacho kilimpatia jina la utani ambalo ni (MWANAMALUNDI).
Hii nikutokana na alipotoka kuzurura na watoto wa majirani zake, walimwambia, “Mamirundi galyo lilihumbura bana bise”, ikiwa na maana "mamiguu yake marefu linarubuni watoto wetu”. Huyu ndo Mwamba Mwanamalundi.
MWANAMALUNDI! alipenda sana kucheza ngoma za jadi, na hii Ilikuwa ni chanzo cha miujiza yake. (Unaambiwa)

Siku moja Mwanamalundi na rafiki zake wawili walikwenda kwa mganga kutafuta dawa ya ngoma  (mvuto) mganga yule alikuwa ni bibi mmoja.
Basi wamefika pale wakamueleza shida yao na wakaamua kwenda porini kutengeneza dawa.

(Unaambiwa) wakiwa porini wakitengeneza dawa, ghafla alitokea myama mbogo  (faru) na kuanza kuwashambulia, mwanamalundi alipanda mtini ili kujiokoa na wale vijana rafiki zake walitimua mbio...
huku bibi yule akisalia pale na kujeruhiwa vibaya na faru yule.

Baadae faru alitokomea, Mwanamalundi akashuka chini na kumkibilia bibi yule na kumbeba begani wakilejea nyumbani kwa bibi yule. Ghafla bibi yule akashuka na kumwambia yule faru Ilikuwa ni mtego tu yaani (ndagu).
Akamsifu na kupata dawa. Huyo ndo ( Mwanamalundi sasa).

Dawa ile Ilikuwa ni chanzo cha miujiza ya huyu mwamba wa kisukuma ( Mwanamalundi) unaambiwa kila shindano alipokuwa akicheza alishinda na kuonesha miujiza mikubwa kuwahi kutokea. Mfano tu.
Mwanamalundi! Alikuwa akicheza ngoma hewani.. bila kukanyaga chini.

Mwanamalundi! Alikuwa akicheza ngoma juu ya chiwe na kuacha alama za miguu yake.

Mwanamalundi! Alipokuwa akicheza ngoma, alikuwa anauwezo wa kujirefusha  na kuwa mrefu kupindukia
Hii ni moja ya miujiza aliyokuwa akiionesha kwenye ngoma. Ukiachilia mbali kujibadirisha na kuwa wanyama tofauti tofauti ikiwemo simba nyati n.k. huu ndo Mwamba (Mwanamalundi).
CHANZO CHA KUKAMATWA NA WAKOLONI.

Mwanamalundi akiwa kijiji cha Nela  (maswa) mkoani Shinyanga. Alipokuwa ameenda kucheza ngoma, jamaa alilogwa na mpinzani wake na kupelekea chakula Chao kisiive kwa masaa kadhaa kitu ambacho si kawida.
Muujiza wa (MWANAMALUNDI) alinyoosha kidole katika poli jirani na kupelekea miti yote kukauka ili wapate kuni, kumbe bahati mbaya kulikuwa na mifugo  (ng'ombe) ya mtemi (Masanja II) ndipo amuru akamatwe.
Walimkamata  (Mwanamalundi ) na kumkabidhi katika serikali ya WAKOLONI, 
Kutokana na miujiza mingi ya kutisha na alivyokuwa akisikika wakoloni walimuomba ili wampotezee jamaa.
Mti kinyonga! Pale mwanza.  Jamaa alikamatwa ili wamnyonge, cha ajabu! Kamba zote zilikatika vibaya kila walipotaka kumyonga Mwamba. Wakoloni wakashindwa. Wakamfunga katika moja ya kisiwa hapo ziwa Victoria
Baada ya Siku kadhaa, wakoloni hawakumkuta Mwamba! Wakasikia yupo kwao kwa mama yake, jamaa wakamfata huko huko kijijini.
Walipfika kabla ya kuondoka. Mwanamalundi alimwachia maziwa mama yake kwenye kibuyu na kumwambia kuwa, angalia maziwa haya siku yakiganda tu! ujue wamesha niua. Lakini yasipoganda ujue badoo nipo hai". Mwamba wakamchukua.
Wakiwa njiani kuelekea Tabora. Wakoloni unaambiwa walitaka awaoneshe miujiza,Mwamba akaanza kazi,alikuasha miti kwa kusonta tu. Waliphisi njaa, Mwamba Alisonta matunda mabichi ghafla yaliiva na kuanza kula. Wakoloni walipagawa, mbaya zaidi alijigeuza kuwashambulia mnyama atakae.
Mwanamalundi! Wakamchukua na kumfunga gereza la kisiwa cha mafia.
Mwamba aliendeleza visanga vyake kule,ikiwemo kupanda viazi,  mihogo na kula kwa muda huo huo,  ikiwemo kutembea juu ya maji kuja bara na kurudi kisiwani tena.Jamaa aliwatesa sana wajerumani!Na kuamua kuwacha tu.
Unaambiwa kuna kipindi jamaa alikuwa anaonekana sehemu tatu. Yaani yupo mafia gerezani,  huyo huyo yupo pahala anacheza ngoma,  na huyo huyo yupo kwa mama yake kijijini. ( Huyu ndo Mwamba Mwanamalundi ).
Wakoloni walikata tamaa kumtafuta, Visanga vyake noma, Alipokuwa akikaa juu ya mawe, anaacha alama za makalio,  miguu,  na muda mwingine alikuwa akicheza bao juu ya mawe na kuacha alama. Mpaka sasa alama hizo zipo, tembelea kahama, Shinyanga na Wilaya za Mwanza utaziona. Zipo..
Mwanamalundi alifariki mwaka 1936s kwa maradhi ya kawaida na kuzikwa Ididí Jihū huko kijiji cha Seke wilaya Kishapu mkoa wa Shinyanga akiwa ana umri wa miaka 40s. Tukio la kifo chake liliitwa "hang'witulo gwa shigela" ikimaanisha "Vita ya kuwakimbia wamasai".
Hii ni kwa sababu wakati Mwanamalundi anakata roho, kulitokea kishindo kikubwa kama tetemeko la ardhi. Watu wengi walikimbia ovyo kwa hofu kuwa labda wamasai wamevamia eneo lao ili kuwaua.
Baada ya kishindo hicho, giza likaingia ghafla, giza ambalo hata kuku wakaanza kurudi nyumbani, fisi wakaanza kutembea mitaani wakidhani ni usiku. Hata baada ya mazishi yake, kaburi lake lilifuka moshi mwingi sana uliopanda mpaka juu mawinguni na kutengeneza giza la muda mfupi.
Mwanamalundi anakumbukwa pia kwa kuweza kutembea hewani bila kukanyaga ardhi, kujibadili na kuwa tofauti kama mnyama, ndege, majani, mti au jiwe na uwezo wake wa kutembea juu ya maji au kuwa ndani ya maji kwa muda mrefu. Huyu ni moja ya watu mashuhuri katika tawala za Kisukuma.
Kuna watu mashuhuri kabla yake kama akina Níndwa, Italange na Sïta. Hawa wote walikuwa ni watu wa miujiza kama alivyokuwa Mwanamalundi.
Makala hii inasimuliwa na Msukuma halisi na mwanahistoria ya Wasukuma Nghwana Ibengwe Shileki Mazege katika kitabu chake kiitwacho "Miujiza ya akina NG'WANA MALUNDI", toleo la kwanza 2015. Huyu ana vitabu vingi sana kuhusu historia ya wasukuma.

Siku Njema Wadau
Cc @DiwaniMsomi
You can follow @HildayaD.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: