Mwl. Christopher Mwakasege - Mambo ya Msingi ya Kutafakari kabla ya kufanya Uamuzi wa Kuoa/Kuolewa.

UZI👇
JAMBO LA KWANZA: Kuoa au kuolewa kunabadilisha uhusiano wako na wazazi wako.
Mwanzo 2:24 anasema, “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili moja”.
Ukiangalia (Zaburi 45:10-11) anasema, “Sikia binti utazame (maana yake anazungumza na msichana) utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie.”
Najua watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi kabisa, unataka kuoa, mwanamume lazima kwanza aachane na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko.
Kuna mabadiliko mahali pakuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako, na mume wako hawezi kuwa baba yako. Mke wako anakuwa mke wako na si mama yako. Mume wako anakuwa mume wako na si baba yako.
https://twitter.com/BarakaSaimon3/status/1249319618377908229?s=19
You can follow @BarakaSaimon3.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: