Nitawapa one true Story.
Nilivyokuwa chalii, nikiwa darasa la sita, pale home palikuwa na kiwanja kwa nje ya fense. Mzee alikuwa anajenga Nyumba ya wapangaji mdogo mdogo. Siku Moja aliukuja jama mmoja na familia yake. Alikuwa na mke na watoto 2.

Akaja kwa mzee na kujieleza kuwa alikuwa hana sehemu ya kuishi, hivyo anaomba ajisitiri katika lile jengo ambalo halijaisha. Wazazi wangu wakajadili wakaona ni sawa. Basi jamaa akaanza kuishi pale na familia yake.
Watoto wa yule jamaa walikuwa wadogo sana, Mmoja alikuwa anatembea labda alikuwa na mwaka hivi, kengine kachanga. Mzee akapambana akaweka bati pale, ili wasinyeshewe. Maisha yakaendelea, nakumbuka nilikuwa nasoma boarding.
Nilivyorudi likizo, nikamwona yule jamaa peke yake akiwa na mtoto. Nikamuuliza mama vipi? Mama akasema mke wake alifariki baada ya kuumwa ghafla. Alilazwa pale mount Meru lakini hakupona. Ukimwangalia jamaa hadi huruma. Amechoka sana.
Wazazi wangu waliendelea kumsaidia yule jamaa, mzee alimtafutia kazi yule jamaa ili aweze kuitunza familia yake. Yule jamaa alishukuru sana. Miaka ikasonga. Wakati niko Form 2, narudi kutoka shule...napata taarifa kuwa yule jamaa alifariki kwa ajali pale mianzini.
Jamaa akaacha watoto wake, wakiwa bado wadogo sana. Na hawakuwa na muangalizi. Baba yangu akasema maneno ambayo mpaka leo sitayasahau, "Watoto hawa ni malaika, na hawakuchagua kupitia haya, hata wewe yangeweza kukukuta"
Mzee aliwachukua wale watoto, nakumbuka usiku wale watoto walikuwa wanalia, na kuita "baba". Walikuwa wanyonge na wenye upole. Na yule mdogo aliuliza, baba atarudi lini?
Baba na mama Yangu, waliwalea wale watoto. Kila nikiwaona nakumbuka wazazi wao. Mimi nikawaita wadogo zangu, nakumbuka mzee alienda kuwatafutia vyeti vya kuzaliwa na kuwapa jina lake.
Mama kwa upande wake, aliwaonyesha upendo wa mama. na kuwapa furaha. Aliwaita wanae, akawalea na kuwa upendo mkubwa. Taratibu wadogo zangu wale wakaanza kuwa na nyuso za furaha. Wakaanza kuruka na kuchangamka kama watoto wengine.
Wakati wa kwenda shule ukafika, wakapelekwa shule. Wadogo zangu wakafurahi sana. tena shule nzuri kama nilivyosoma mimi!
Wakaingia mioyoni mwetu, wakawa ndugu zangu wa kweli. Sasa hivi wako sekondari, Ni wadogo zangu na nawapenda hakuna mfano.
Somo;
upendo huponya na kuleta tumaini jipya, upendo hufufua nafsi zilizokufa na kuzipa dira ya maisha. Ubinadamu na upendo ni utajiri mkubwa sana. Ona leo nina wadogo zangu, wakati mimimkwetu nilizaliwa peke yangu. Ila upendo umenipa wadogo zangu.