Kutana na baba aliyeua familia yake, na kupotea kwa miaka 18.
________________________________

Baada ya kutoa pumzi ya kila mmoja, alisafisha sakafu iliyokuwa imetapaakaa damu na kujiandalia chakula cha usiku mezani, ambapo roho moja tu, ndiyo iliyokuwa hai kula. Alipomaliza,
akaosha vyombo na kuvirudisha sehemu yake, kisha akalala - yeye kitandani; familia yake ambayo sasa walikuwa marehemu, walilala sakafuni wakiwa ndani ya mabegi ya kulalia.

Hakika ukistaajabu ya mwafrika, utashangaa ya mzungu! Yule anamchoma mkewe kwa magunia mawili ya mkaa; huyu
anaangamiza familia yake kwa bunduki. Basi tu, ni ndani ya hii dunia ambayo gwiji na mwandishi wa kazi za fasihi, marehemu Euphrase Kezilahabi, aliita ni "Uwanja wa fujo". Ambamo ndani yake kila mtu akifanya fujo yake - ya amani; ama ama isiyo ya amani. Lakini kuna fujo nyingine,
hata huyu shetani tunayemlaani, anaziogopa, basi ni mfano wa hii la John List, baba aliyeua familia yake na kupotea kwa badili utambulisho wake. Hakika, kuna matumbo mema ya mama zetu, yamepata kuzaa mashetani!

Naam, mnamo tarehe 9 Novemba, 1971, katika mji wa Westfield,
New Jersey, Marekani, ilikuwa ni kiza kwa familia ya John List. Siku hiyo, ambayo kama inavyokuwa kawaida kwa baba yoyote yule kuamka asubuhi na wanawe, ilikuwa tofauti kwa John List aliyekuwa na umri wa miaka 46 kwa wakati huo. Akiwa na mpango ovu kwa siku hiyo, mpango aliokuwa
anaufikiria kwa muda wa mwezi mmoja kabla, kichwani mwake. Aliamka kama afanyavyo siku zote na kupata kifungua kinywa na wanawe watatu - Patricia, aliyekuwa na umri wa miaka 16; John Jr., aliyekuwa na umri wa miaka 15; na Frederick, aliyekuwa na umri wa miaka 13. Walipata
kifungua kinywa taratibu na stori za hapa na pale huku akiwa makini sana kuepusha kushukiwa jambo na familia yake juu ya mpango wake ovu wa siku hiyo. Masikini, hakuna aliyeweza kujua kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kwao kupumua, bali ni muda tu ulisubiriwa ufike.
Ndiyo, ni kabla ya madhila haya, maisha ya familia hii yalianza kuingii gizani siku John alipokutana na kipenzi chake, Helen na kuanzisha mahusiano ya kimapenzi. Helen, alikuwa mjane pindi alipoanzisha mahusiano na John. Alimdanganya John kuwa ni mjamzito, hali iliyofanya ndoa
ifungwe haraka. Baada ya ndoa, ndipo Helen akamwambia hakuwa mjamzito, ila alimdanganya John ili wafunge ndoa. Ni jambo amabalo halikumpendeza John, ila atafanya nini na imani yake hairuhusu kuvunja ndoa. Lakini alifanya kitu. Alimzalisha Helen waototo watatu ndani ya miaka mnne.
Na hapo jukumu la kulea familia likawa kubwa na juu yake.

John ambaye alikuwa na taaluma ya uhasibu, alikuwa anafanya kazi katika benki moja hapo New Jersey. Uchapakazi wake ulikuwa hauna dosari. Kwa haiba alikuwa mtaratibu. Lakini kasoro yake kubwa alikuwa ni mtu wa misimamo
jambo lililopelekea kutokea migogoro kati yake na; bosi wake na wafanyakazi wengine hali iliyofanya apewe likizo mara kadhaa.

Naam, kila mtu ana mlango wake. Mambo yalianza kunyooka baada ya John kupandishwa ngazi na kuwa makamu wa Rais wa benki. Hakika hii ndiyo nafasi Helen
aliisuburi kwa hamu. Alianza kumshinikiza mumewe wanunue nyumba ya ndoto yao ya muda mrefu. Nyumba ambayo ilipewa jina la "Breeze Knoll", ambayo ilikuwa na vyumba 19 na ikiwa katika maeneo ghali zaidi mjini hapo. Ndiyo, ni hulka ya wanawake wengi kupenda vitu vizuri na maisha
mazuri kwa familia zao. Na hususani kwa mwanamke ambaye hana kazi ya kipato, basi presha huwa kubwa kwa mwanaume kutimiza mapendekezo ya mwanamke. Ndiyo, mama ni roho ya familia; baba ni kichwa cha familia. Japokuwa jambo hili liliwapelekea kugombana mara kadhaa.

Basi kwa
kuwa John alikuwa na mahusiano mazuri sana na ya karibu na mama yake aliyeitwa Alma, tofauti na yalivyokuwa kwa marehemu baba yake, basi aliamua akope pesa kwake ili atimize ndoto ya kuinunua nyumba hiyo. Ili aazimwe pesa, makubaliano yalifanyika kati ya John na mama yake kuwa
endapo nyumba itanunuliwa, basi mama yake ahamie kaika 'apatimenti' ya ghorofa ya tatu, na wao wabaki na ile ya chini na ya pili. Walikubaliana, na nyumba iliponunuliwa wakafanya hivyo.

Baada ya kuhamia katika nyumba hiyo, mambo yalianza kwenda mrama. Haikuchukua hata mwaka,
John alifukuzwa kazi benki kutokana na mgogoro kati yake na; bisi wake na wafanyakazi wengine. Sasa badala ya kukubali udhaifu na kuieleza familia yake jambo hili ili wakubaliane na hali, alificha. Lakini kila siku aliamka asubuhi kama kawaida, alivaa na kuwasha gari yake
akiaga kama anakwenda kazini. Badala yake alikuwa anakwenda hadi kituo komoja cha treni, akifika, anageuza gari yake kwenda kituo kingine ili kuvuta muda(buy time). Na alifanya hivi kila siku hadi siku alipopata kazi nyingine ya malipo madogo, ambayo nayo hakuchukua muda,
alifukuzwa. Kweli ukizoea mabo makubwa, madogo huwa ni mapuuza! Ndivyo ilivyokuwa kwa John, huenda alidharau kazi za malipo madogo na ndio maana hakuweza kudumu kwenye kazi hizo. Na sasa gharama za maisha zikawa kubwa mno kuzimudu, hali iliyompelekea kuanza kukomba pesa zilizo
pesa zilizo kwenye 'akaunti' ya mama yake bila ya yeye kujua. Hadi kufika mwaka 1971, mwaka wa tukio, John alikuwa amefilisika, msharika wa wa Kilutheri aliyeamini kuwa masikini ni dhambi.

Jambo hili lilianza kumchanganya, kwa mtu ambaye sasa familia yake ilikuwa imeonja
maisha mazuri, ilikuwa inamtazama yeye. Na zaidi akiwa mtu wa misimamo ya kidini, aliwafikiria wanaye ni jinsi gani atawaepusha na dhambi ya dunia. Watoto ambao walikuwa 'matineja'na damu zikichemka katika maisha ya kila aina ya starehe na uhalifu Marekani. Zaidi, alimfikiria
binti yake Patricia, ambaye alielezea ndoto yake ya kuja kuwa muigizaji siku moja, fani ambayo kwa John ilikuwa ni ya kishetani. Achilia mbali kunesha dhamira ya kuwa muigizaji, bali kulikuwa na fununu kuwa binti huyo anatumia bangi. Lakini hili la Patricia halikuwa zito hadi
sana hadi kufikia kuiangamiza familia yake.

Afya ya mkewe ilizidi kuzorota kwa haraka. Na Helen ashukuru kwa siri aliyomficha mumewe kwa miaka yote. Kwani kwa baadaye alianza kujisikia uchovu na kupoteza uoni katika jicho lake la kulia, ambapo majira ya baridi mwaka 1969, Helen
alipimwa na kukutikana na ugonjwa wa kaswende ambao aliupata kwa mwanaume aliyekuwa naye kabla ya kuwa na John. Akawa mnywaji sana wa pombe na mtegemezi wa dawa za kutuliza akili(tranquilizers). Jambo lililochochea mawazo maovu kwa John, ni pale mkewe alipoacha kabisa kwenda
kanisani, yawezakana kutokana na mvurugiko wa akili.

Yote haya yalikuwa yanachemka kichwani mwa John. Ni jinsi gani ataiepusha familia yake na aibu ya umasikini kutegemea misaada ya serikali, na dhambi za ulimwengu. Ilikuwa ajiue yeye, lakini kutokana na imani ya dini yake,
kujiua ni dhambi isiyosameheka. Basi akahitimisha mawazoni mwake, ni kuiangamiza familia yake tu. Na hili alikuwa analifikiria kwa muda wa mwezi mmoja ni jinsi gani atatimiza lengo lake ovu.

Basi, majira ya asubuhi ya siku hiyo ya maauaji ya tarehe 9 Novemba, 1971, kwa mujibu
wa vyanzo vingi vilivyo andika kisa hiki. Ni wakati watoto wote wamekwenda shule na kazini. Mkewe, Helen wakati huo akiwa na umri wa miaka 46 sawa na mumewe, kama kawaida alikuwa ameamka na kuja 'floo' ya chini kwa ajili ya kuandaa kahawa. Aliingia jikoni kuwasha jiko kisha
akainjika birika la kahawa huku John akimsemesha stori mbili-tatu ili kumzuga. Baada ya kahawa kuchemka na kuzima jiko, alijimiminia na kwenda kuketi mezani upande ambao mwanga wa jua unaingilia dirishani na kumpa joto. Kwa wakati huo Helen hakujua, John alikuwa na bunduki mkono
wake wa kulia aliyopewa na marehemu baba yake aina ya "9mm stayr pistol", alimsogelea taratibu mkewe aliyekuwa amempa mgongo. Helen lihisi miondoko ikimjia, aligeuka taratibu ili amtazame mumewe kama vile mwanamke anaye pokea busu ageukavyo. Loo! Ilikuwa ni risasi ilifyatuliwa
na kumpata kwenye taya. Alianguka chini kwa mshindo. Helen tayari alikuwa chini amelala, sura imetazama sakafu huku damu ikimiminika na kusambaa hapo chini ya meza. Na chumba cha jiko chote kikanuka harufu ya mripuko wa risasi. Helen alitulia, alikata kauli. Aliuweka mwili wake
mwili wake ndani ya begi la kulalia, na kumburuza hadi chumba cha kucheza muziki na kumuacha hapo sakafuni.

Baada ya kumaliza kazi ya kinyama kwa mkewe, safari hii ilikuwa ni kupanda ngazi juu hadi katika 'apatimenti'ya mama yake mzazi, Alma - mama wa umri wa mika 84 kwa
wakati huo. Na kwa wakati huo Alma alikuwa najiandalia kifungua kinywa. Kweli John hajawahi ingia katika 'apatimenti' ya mama yake bila hodi, bali sasa ilikuwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo. Masikini, mama yake alikuwa pembeni ya jiko la kuoka mikate na siagi yake mkononi ndani
ya sahani. Akimtazama mwanaye aliyekuwa amefungua mlango akimjia. Alma akamuuliza mwanaye, "hiyo kelele ni ya nini huko chini?". Bila kujibu, alinyanyua bunduki na kumpiga juu ya jicho lake la kushoto. Kisahani cha siagi mkononi kikadondokaka chini sanjari na mama mzee sakafuni
juu ya malumalu. Huyu ni mama yake mzazi! Ndiyo, ni mama mzazi aliyemleta duniani!

Alifikiria amburuze hadi 'apatimenti' ya chini, akaona ni kazi ngumu. Alma alikuwa ni mwanamke mwenye mwili mkubwa, si mnene, bali mrefu na mwenye mifupa mizito. Hawezi kumburuza mbali hadi
chumba cha muziki chini; wala hawezi kumuacha amelala hapo. Alikumbuka zulia la plastiki mlangoni kwa mama yake, basi akalichukua na kumuweka humo, kisha akamburuza hadi kwenye korido. Aliendelea kuhangaika, aliuvuta mwili hadi sehemu inayohifadhi maji ya mvua, na hapo
akamsafisha damu. Na baad ya kumaliza, alisafisha damu ndani ya nyumba akitumia gazeti la "Sunday News", lakini akaona halifai. Alichukua taulo kuu kuu akalitumia kusafisha damu kisha akamfunika nalo usoni. Hangaika yote hii si kwamba alikuwa anaficha kitu, balia alikumbuka
mafundisho ya mama yake, usafi, kujitunza na heshima alivyokuwa anamsisitizia.

Alipomaliza kwa mama yake, alirudi tena 'apatimenti' ya chini alikolala mkewe mauti. Nako alifanya usafi jikoni. Akajipanga kuendelea na uovu wake. Alipiga simu kwa waalimu na mabosi wa wanawe
akidanganya kuwa watahitaji kuondoka kwa siku kadhaa kwenda North Carolina kumuona mama yake Helen ambaye ni mgonjwa. Alikwenda haraka posta kutuma barua ili kusisitiza jambo hilo, lakini yeye akazuia kupokea barua yoyote. Alikwenda mbali zaidi, alisimamisha huduma ya maziwa ya
kila siku, na huduma ya magazeti. Hakuishia hapo, alikimbia haraka benki na kutoa kiasi cha dola 2000 ambayo ilibaki kama "saving bond". Aliporudi, alijiandalia chakula(sandwich), akila taratibu huku akuwasubiri wanaye warudi.

Wakwanza, alikuwa ni Patricia, ambaye kwa bahati
mbaya ya kutojua, alimpigia baba yake simu na kumwambia alikuwa anajihisi mgonjwa, hivyo John aliwasha gari yake na kwenda kumchukua. Walipofika nyumbani na kuingia ndani, John akitumia bunduki yake nyingine aina ya ".22 pistol", alimfyatulia risasi binti yake juu ya taya na
kumuua papo hapo. Naye aliwekwa ndani ya begi la kulalia na kuburuzwa hadi chumba cha muziki alikowekwa Helen. Hakuchelewa, akapiga simu kazini kwa Frederick, KMV Associates, na kuomba kuongea na Fred ambapo alimpasha habari ya kuumwa kwa Patricia. Karani wa KMV Associates,
Margaret Koleszar, anakumbuka maneno aliyoongea Frederick alipokuwa anaongea na baba yake kwa simu, "Nini kimempata Patty? ". Kisha akaondoka kazini hapo kwa haraka akiwahi nyumbani.

Wakati huo John alipanga kwenda kumchukua Frederick, lakini kabla hajaanza kuondoka

PART 2...
You can follow @OscarMwaisoloka.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: