Ushawahi kujiuliza kuhusu Pixels au Resolution zina maana gani? Au kwanini video kwenye simu ipo clear lakini ukiiweka kwenye TV au laptop inapungua QUALITY? Ushawai kujiuliza hizi namba zinamaanisha nini 1080, 720, 480, 4k..etc

Nifuate, Nikujuze!!

THREAD by #adamphoneclinic
Kitambo screen resolution haikua issue sana, screen zilikuwa zinakuja na resolution preset na kama ukitaka higher resolution au rangi au vyote kwa pamoja ilikuwa una install drivers kwa ajili ya video card then you move.. Hebu tuanzie mwanzo, tupate uelewa kuhusu hili...
Teknolojia ya Kioo chenye rangi ilianzishwa na IBM ambapo ilikuwa released kwa mpangilio huu...
1. CGA- Color Graphics Adapter
2. EGA- Enhanced Graphic Adapter
3. VGA- Video Graphic Array
Tazama picha hapo chini, huu ndio ulikuwa muenokano wa CGA display, yeaah tumetoka mbali๐Ÿ˜ƒ
Zamani zaidi kabla ya hizi teknolojia, tulikuwa na screen za black and white ila IBM walileta mapinduzi ya rangi kwa kuleta CGA kisha EGA na baadae VGA.

PIXELS and RESOLUTION
Tuanzie hapa kwanza, pixels ni nini? Pixels ni unit ndogo kabisa picha ya dijitali au graphics ambayo kwa muunganiko wake huleta picha au video iliokamilika. Chukulia mfano wa unga wa ngano, zile punje ndogo ndogo kabisa ambazo zikiunganishwa pamoja huleta unga kisha tupate keki
So, this is what happens: Tukiwa kwenye mfano wa unga wa ngano, kwa jinsi unga ulivyo mwingi ndivyo keki itakua kubwa sawa na vile unga ukiwa kidogo basi keki huwa ndogo. Muunganiko wa pixels ndio huleta ubora wa picha, kadri pixels zinavyokuwa nyinigi ndio picha/video huboreka.
Pixels hubeba information muhimu kama rangi na uang'avu wa picha au video. Wingi wa pixels ndio huleta vitu kama HD, 4k, 8k e.t.c na uchache wake ndio utapata zile video au picha ambazo mchana kama usiku๐Ÿคฃ ...

Hebu tuzungumzie Resolution
Resolution: Jumla ya pixels kwenye image au video (japo neno la resolution hutumiwa interchangeably na ppi-pixels per inch). Tumezoea kulitumia neno Resolution kama jumla ya Pixels kwenye display, mfano 480 x 640 =307,200.
Ushawahi kukutana na screen zimeandikwa 1080p na 1080i? au 720p na 720i? Unaelewa maana zake?
p-progressive
i-interlaced

Interlaced-ni mpangilio wa pixels horizontally, hii mistari ilikuwa inaonekana kirahisi kama ukitumia zile screen za kitambo ila kwa vioo vya sasa.
Ngoja nikuelezee kwanini screen za sasa ni ngumu kuona mistari. Wataalamu walijitahidi namna ya kufanya ile mistari isionekane then wakaja na hii progressive scan. Screen inafanya painting juu ya ile mistari, kitendo cha haraka kiasi kwamba hata macho ya mtazamaji hayawezi kuona
720p, 1080p, 1440p, 2K, 4K and 8K?
720p =1280 x 720 - inafahamika kama HD au "HD Ready" resolution
1080p = 1920 x 1080 - inafahamika kama FHD au "Full HD" resolution
1440p = 2560 x 1440 - inafahamika kama QHD au Quad HD resolution na mara nyingi hutumika katika gaming monitors na high-end smartphones

4K au 2160p = 3840 x 2160 - inafahamika kama 4K, UHD au Ultra HD resolution. Bonge moja la resolution, inapatikana kwenye TV na monitors za pc
Halafu kuna baba lao kwa sasa, 8k
8K au 4320p = 7680 x 4320 bahati mbaya sana huu mzigo clarity yake unaweza ipata kwa TV screen za Samsung na LG ambazo ni gharama sana. Nafikiri kutokana na maelezo yangu unaweza pata picha how clear this TV is...
Kwenye swali la msingi, Je unaweza kuangalia video ya 2160p kwenye device yenye resolution ya chini? Yes, inawezekana ila hutaweza kuona ile quality yake kama ambavyo mwenye display ya size yake.
Kuna mengi sana ya kuzungumzia na kujifunza kuhusu pixels na resolutions ila kwa leo wacha niishie hapa.

Incase umepishana na thread zangu nyingine tafadhali check my pinned๐Ÿ“Œtweet, ina thread zangu zote.

cc @Abbymexahnk
You can follow @adam_adyz.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword โ€œunrollโ€ to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: