Tonsillitis ni maambukizi katika vifuko vidogo vya limfu (tezi limfu) vilivyoko kinywani viitwavyo tonsils. Vifuko hivi vina seli na chembechembe muhimu katika kupambana na maambukizi ndani ya kinywa.

Fuatilia uzi 🧵
Maambukizi kwenye tonsils husababishwa na virusi au bakteria.
Kuna aina mbili za maambukizi kwenye tezi za tonsils:
-Acute Tonsillitis: Haya ni maambukizi ambayo hudumu kuanzia siku 4 hadi wiki 2. Mgonjwa anakuwa na homa kali, koo kuwasha na maumivu wakati wa kumeza.....
Hii huwapata hasa watoto kuanzia umri wa miaka 2 hadi 15. Uchunguzi ndani ya kinywa huonyesha tezi kuvimba na kuwa nyekundu.

Matibabu yake utegemea na maambukizi yanatokana na virusi au bakteria baada ya daktari kufanya uchunguzi.
Chronic Tonsillitis: Haya ni maambukizi kwenye tezi za tonsils yanayodumu zaidi ya wiki 2. Uchunguzi wa kinywa uonyesha tezi kuvimba na kuwa nyekundu, vifuko vya usaha kwenye tezi(bacterial tonsillitis) na kutoa harufu mbaya mdomoni.
Maambukizi ya bakteria kwenye tonsils huweza kutibiwa kwa dawa (antibiotics) baada ya daktari kuchukua kipimo cha swab kwenye usaha ulioko kwenye tezi na kujua ni aina gani ya bakteria wameshambulia tezi. Kwa virusi(viral tonsillitis) matibabu yake ni kutibu dalili km homa n.k
Kwa watoto wadogo, tezi za tonsils (na tezi nyingine zinaitwa adenoids) zinaweza kuvimba na kusababisha njia ya hewa kuziba na mtoto kupata homa za mara kwa mara, kukoroma sana usiku na wakati mwingine kuamka usiku ghafl kwenye usingizi ili apumue.
Matibabu ya moja kwa moja kwa maambukizi sugu yanayojirudia(Recurrent tonsillitis), au kusababisha njia ya hewa kuziba hasa kwa watoto ni kufanyiwa upasuaji wa kutoa tonsils.
You can follow @Barongo01.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: