Mimi binafsi sifurahishwi na huu mfumo wa uchangishaji pesa kwenye harusi! Naona kabisa KUOA ni suala la kujipanga, unakua na muda wako umeupanga kabisa kwamba kufikia kipindi fulani mimi nitakua naingia katika hiki kitu (ndoa). Nguvu za kuimizana kuchangiana katika harusi

Tungeziwekeza pale tunapopata majanga mfano kuuguliwa, misiba, labda mafuriko, kushindwa kulipa Ada na vingine viendanavyo na hivyo ingeleta maana. Sipingi watu kuchangiana na niko tayari kumchangia mtu yeyote yule atakaeniomba nimchangie ili afanikishe harusi yake. Sambamba na

Hilo pia sioni haja ya watu kujazana kwenye sherehe, wengine wanadhani kwamba wingi wa wahudhuriaji kwenye sherehe ya harusi ndio kunogesha. Napingana na hili kabisa, kuna mifano miwili inayomuhusisha Kaka Yangu @Stimellah naomba niitumie,wakati anapanga ishu ya kuoa aliniambia

‘Junior Mdogo wangu chochote kile unachopanga kukifanya tambua ni chako, maamuzi yoyote yale unayofanya jua ni yako, haijalishi ni ya aina gani kumbuka ni ya kwako wewe sio mwingine’ Leo hii nina mpango wa kuoa, Ninaoa mimi sio Family wala marafiki, hii ni kwa ajili yangu mimi

Hivyo basi nitapambana kadri ya uwezo wangu kufa kupona nihakikishe hili linafanikiwa. Baada Siku kadhaa akaniambia dogo am done now, jiandae na Shughuli. Sasa siyo kwamba hawakuwepo ndugu,jamaa na marafiki wa kuchangia, sio kwamba Family haina pesa ( Pesa ipo nyingi tu) lakini

Shughuli sio ya familia ni ya kwake yeye na sio kwa kuwa ana pesa sana But ni yeye ndo muhusika wa Shughuli. Mfano wa pili kwenye harusi tulipanga wageni wawe 200 but mbaya/zuri zaidi wageni walikua mara mbili zaidi wengine hatujui walitokea wapi, na wote wakala na kunywa plus

Kusaza. Bila ya kumchangisha mtu yoyote yule. Sasa iweje watu wengine wanategemea michango ndo wafanikishe harusi zao? Huu utamaduni utakufa lini? Mambo ya kuchangishana haya ndio yanafanya dharau zinaanza,mke hawi wako tena anakua wa jumuiya kila mtu anamzungumzia atakavyo

Kisa tu alichanga kwenye harusi, kwani ameolewa na ukoo? Kaolewa na marafiki? Muda mwingine mtu Una uwezo wa kufanya sherehe yako ndogo tu but kwa kuwa Unataka sifa uzungumziwe kwamba fulani harusi yake ilifana but deep down madeni plus michango mingi umeacha nyuma yako

Harusi inaisha tu unaanza kuugua kwa stress. Bro fanya kitu kilicho ndani ya uwezo wako/familia yako, hawa wanaokuchangia wengi wao ndio wabaya kabisa hawana jema na wewe ukimaliza tu wanaanza kukuzungumzia vibaya. Tubaki tu kuchangiana kwenye matatizo lakini sio kwenye

Sherehe. Mwaka Jana ndugu yetu @EA1adams aliugua figo,kongosho & Ini akapelekwa kwenye matibabu USA
kwa ajili ya matibabu but hakuna rafiki ata mmoja wale waliokua wanajifanya wanae sana wengi wao wakiwa humu aliemchangia ata sh 100 wengine ata kumjulia hali, mbaya zaidi


Wengi wao ndio waliozidi kucheka na kufurahia kuugua kwake, lakini ingekua harusi Au pesa za kula Maison fasta wangetoa. nikajifunza kwamba hakuna mtu atakae kujali wakati wa shida/unapoishiwa pia hivyo basi pambana kadri uwezavyo. God is great Elly is doing good but also Dave

Alifanikisha harusi bila kumchangisha mtu yeyote yule,sasa wewe jifanye unafurahia ooh they’re my friends ngoja wanichangie. My Nigga Ipo siku mkeo atakua mke wa Jumuiya, Nijipange zangu hapa nimuoe Viola wangu sasa na mimi. halafu msichukie ni ushauri tu nawapatia.