'80 chapatis gone in 10seconds' Thread...
So siku ni sunday tumeamka vizuri hangdown kidogo tu ...
Before service kulikua na kale ka prep ka 7 sijui hadi 9.Kama kawaida hakuna kitu tunafanya isipokua kuskiza palito ama kulala..
Preps ziliisha kama tumeruka services .praise and worship mdogo mdogo..
On sundays tulikua tunakula Lyonnaise potato,frijol with a pinch of salt served with chapati. So tukiwa tu service kaharufu ka chapo kalitupiga mbaya sana tukaanza kujadiliana na beshte yangu vile tunaweza ziendea
Beshte yangu let me call him 'brayo' akanishow cooks wakitoka kuenda kuserve lunch twende tupite nazo but since nilikua najua hazitakua mob nikamshow.....
Service iliisha kama tumeenda lunch.Hio saa bado tunapanga tu vile tupiga hio shughuli ...
Crowd ya chapo heist ilianza kuongezeka ikabidi akina johnte kevo ndani kwa mix so plan ikakua brayo aingie na roof juu ni mdogo and he got the skills .So vile cooks walitoka kuenda kupumzika shughuli nayo ikanoga
Jamaa ilipanda roof design ya Spiderman na akapenya akaenda kufungua dirisha flani kubwa ungedhani ni mlango .Tulikua tunangalia ndani tunaona machapo tunasmile tu
Kitchen ilikua Karibu na swimming pool na bado hapo kando ndio tulikua tunafulia nguo .Tuchukua bucket moja tukajaza machapo kama tumefunika na nguo kama tumestyep
Brayo btw alitoka na hio window alafu akafunga na nje ndio kusionekane kulikua na mtu ndani
Tulikua tuchukue hadi mikate na bb but hio tuliamua tutaishughulikia siku ingine and funny enough it happened (story for another day)
So ndio hao sisi kwa dorm .Chapo ni mingi ata hatuwezi maliza .Unakula chapo ukiteremsha na chapo ingine😂😂😂 ilibidi tumeita mafans bana..
Zile zilibaki ilibidi tumezifunganisha na manguo tukaziweka kwa paper bag kama tumeziweka ndani ya tank ya huko juu saa zilikua zinahang tu.
Punde si punde tukaona cooks Ati ndio wanarudi kitchen kumalizia round 2
Ghafla bin Vu punde si punde Kile hawakutambua ni chapati kwisha pata miguu na meno za kuzitafuta.lahaula iwejeeeeeee😂😂😂
Walimo ingia mumo ndani walipatwa na mshangao Kwa kweli, wahenga hawakutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa waliponena, paka akitoka panya hutawala ndio ndivyo ikakua wenzangu.
Cooks walibaki hapo wameshangaa tu wakijiuliza maswali😂😂😂
Mmoja wa had cook alikua anaitwa waJohn alitoka amejaa ngori😂😂😂
Dorm inspection ikifanywa haraka upesi hawakupata kitu ikabaki wamenunua unga na pesa zao wakaanza tena afresh saa hizo tunararua machapo kama nonsense
Boarding master alikua anakujia information kutoka kwetu tunamwambia tu....
Monday ilifika na highlight ilikua '80 chapatis gone in 60 sec' Fast forward no one was caught so we were just there like....
THE END.
You can follow @edikomunga.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: