#ElimikaWikiendi Tuongee Teknolojia 💻 📱
Moja ya mambo mazuri yanayotokea siku hizi ni vijana wengi zaidi kujikita kwenye ubunifu kwa kutumia teknolojia. Binafsi huwa nafurahi ninapopata message za watu wakitaka kujua namna ya kufanyia kazi mawazo yao ya ubunifu. Hivyo huu uzi utahusu hilo. #ElimikaWikiendi
Kuna mambo kadhaa ya kuyazingatia. Moja, idea haina thamani yoyote. Kila mtu ana ideas. Kinachotia thamani ni utelelezaji. Kuna kasumba ya “nikisema nitaibiwa idea yangu”. Ingawa kuna ukweli katika hili, huwezi kutamia idea na wengine wakuangalie tu. #ElimikaWikiendi
Pili, katika kutekeleza idea usisubiri mpaka uwe za kila kitu ili uanze. Wanasema kwenye safari ya ubunifu usisubiri mpaka uone ngazi yote. Ukichukua hatua ya kwanza vichane vingine vyote vitaonekana. Baada ya kusema hayo, Tuangalie namna ya kuanza. #ElimikaWikiendi
Idea yoyote (haswa ya kiteknolojia inabidi ianzie na ielekewe kwenye karatasi kwanza kabla haujaanza kuifanya. Kabla haujatengeneza logo na matshirt na Instagram account, iandike. Katika kuiandika, nashauri utumie nyenzo inaitwa Business Model Canvas. #ElimikaWikiendi
Business Model Canvas (BMC), ni nyenzo inayotumiwa na wabunifu wote duniani katika kuyafuma mawazo yao, lakini pia katika kuyaelezea mawazo yao. Nitaomba leo nielekeze namna ya kuitumia. Tuwe wote. #ElimikaWikiendi
Kipengele cha kwanza cha BMC ni Value proposition. Kiufupi, hapa inabidi ueleze unafanya nini na unachofanya kina thamani gani. Kuelezea hili kwa ubora zaidi, tuchague sekta ya kuitolea mfano wa wazo. ( @ElimikaWikiendi naona nitachukua zaidi ya 30 minutes leo 😬) #ElimikaWikiendi
Sawa, wengi mmechagua Kilimo. Sasa, tufanye idea ni kwamba umegundua wakulima wengi wanashindwa kupata wateja wa mbali na hivyo kupata hasara. Idea ni kutengeneza mfumo utakaomwezesha mkulima kuuza mazao kutoka shambani bila kuhitaji dalali. #ElimikaWikiendi
Jambo la kwanza baada ya hili ni kujiuliza: nini tunachikijua kuhusu huyu mkulima: -
1. Ni wa saizi ya chini au ya kati
2. Hana smartphone/hajui Internet kwa upana wake
3. Yupo kijijini.
4. Elimu yake sio ya juu

Idea yetu inabidi izingatie haya yote. #ElimikaWikiendi
Hatimaye, idea yetu rasmi ni mfumo wa mkulima kuuza mazao bila kuhitaji Internet au Dalali. Mfumo utafanya kazi kwa SMS, mkulima atatuma message ya anachouza, kitapostiwa kwenye mfumo na watu wataweza kuona. Sasa tunaweza kuanza kujaza Value Proposition. #ElimikaWikiendi
Value proposition sio unachokifanya WEWE, ni faida zipi anazozipata mlengwa wako. Kwa idea yetu, value proposition zetu ni:-
- Kuongeza faida kwa mkulima kwa kuondoa mtu wa kati
- Kupanua wigo la wateja kwa mkulima kwa kumuunganisha na wateja wa mbali
1/2 #ElimikaWikiendi ..
- Kuwasaidia wateja kupata mazao fresh moja kwa moja kutoka shamba.

Unaweza kuzifikiria nyingine. Mara nyingi katika hatua hii ndio unaenda vijijini kuongea na wakulima moja kwa moja kujua changamoto na faida za ziada za solution yako. #ElimikaWikiendi
Kipengele cha pili ni “how do you do it?”. Hiki tayari tumeshaanza kukijaza. Hapa ndio tutaanisha kwamba tuna mfumo wa mkulima kuweka mazao kwa SMS, na kupokea orders kwa njia hiyo hiyo. Ila pi, kwa uzoefu wangu tayari kuna maswali magumu tayari yanakuja hapa: #ElimikaWikiendi
Moja, kwa kuwa huu mfumo unafanya kazi kwa sms, kama mteja nawezaje kujihakikishia quality ya mazao na hata picha siioni?
Pili, malipo yanakuwaje? Baada au kabla? Kama kabla, inakuwaje mkulima asipotuma mazao? Kama baada, je mazao yakiwa ya uongo au low quality? #ElimikaWikiendi
Hapa inabidi tuweke mfumo wa verification (kama Twitter wanavyofany na blueticks zao). Tunakuwa na agents kila mkoa ambapo mkulima anapojisajili, agent wa huo mkoa anaenda kuhakikisha shamba na quality kisa usajili wake unahitimishwa. #ElimikaWikiendi
Pili, inabidi tuweke mfumo wa kupeana nyota kama wa Uber na Taxify. Mkulima akiuza bidhaa mteja anampa nyota. Lakini pia kuepuka wateja wasumbufu mkulima pia anampa nyota. Yaandike haya kwenye hiki kipengele. Haya yote binafsi najua yanawezekana kwa SMS. #ElimikaWikiendi
Kipengele kinachofuata ni cha resources. Unahitaji nini ili uweze kufanikiwa kwenye mawazo haya (usiwaze hela 😒). Hapa kwanza tunajua tunahitaji:
- Maagent
- Wataalamu wa kutengeneza mfumo
- Office
- ..mengineyo (unaweza kufikiria vingine)

Utajaza hapo. #ElimikaWikiendi
Kipengele kinachofuata ni “What will it cost?” Hapo sasa ndio utawaza kwa hela. Unaangalia yale mahitaji tuliyoyalist hapo juu yanacost kiasi gani. Fanya research kwa kila hitaji kisa upate namba ya kila hitaji. #ElimikaWikiendi
Kipengele kinachofuata ni “how will you reach them?” Unawafikiaje wateja wako? Hapa kuna matangazo kwa njia ya redio, kuwatembelea moja kwa moja mashambani, kuongea kwenye mikutano ya vijiji, you get the idea. Fikiria njia nyingine uzijaze. #ElimikaWikiendi
Baada ya hapo tunaangalia “How do you interact with them?” Hiki kinafanana na kilichopita isipokuwa hiki ni kwa wale ambao umeshawapata na tayari wanatumia huduma yako. Unawasilianaje nao? Unaweza kuweka namna ya kutoa feedback au kuwa na namba ya customer care. #ElimikaWikiendi
Tukitoka hapo tunaenda kujibu “Who will you help?”. Kimsingi kama unalenga watu wote basi humlengi yoyote. Hapa inabidi uwe specific ni mkulima wa aina gani unamlenga. Kwa sisi tayari tulishadefine awali (mkulima wa chini/kati). Unaweza kuwa specific zaidi pia #ElimikaWikiendi
Baada ya hapo, turudi upande wa kushoto kuna kipengele cha “who will help YOU?”. Hapa angalia mashirika au watu ambao wangependa tatizo unalosolve liondoke au wanaweza kufaidika na ubunifu wako. Wizara ya kilimo, makampuni ya simu, umoja wa wakulima, etc #ElimikaWikiendi
Mwisho, unaainisha namna utatengeneza hela. Ubunifu wowote, hata kama ni wa kiharakati inabidi ujiendeshe. Unatengenezaje hela? Unaweza sema utachukua 5% kwa kila muamala, au pia malipo ya uanachama ya mwezi. Fikiria zaidi. Hili nalo ni darasa jingine kabisa. #ElimikaWikiendi
Ukitoka hapo unatengeza document yako nzuri unaanza kuifanyia kazi. Hatua ya pili kutoka hapa ni kutengeneza kitu wanaita MVP (Minimal Viable Product). Hii ni ubunifu wako wa awali kabisa ambao hauna mbwembwe nyingi ambao watu wanaweza kuutumia. #ElimikaWikiendi
Ukiweza kupata at least watu kadhaa wakatumia wakakupa feedback kisha ukaboresha, hivyo ndio namna wazo na ubunifu wako unakuwa. Baadae unatengeneza pitch deck yako nzuri kisha unatafuta investors wa kukusaidia kukua. Hili ni darasa tutakuwa nalo siku nyingine. #ElimikaWikiendi
Mbaki salama.

- Given.
You can follow @GIVENALITY.
Tip: mention @twtextapp on a Twitter thread with the keyword “unroll” to get a link to it.

Latest Threads Unrolled: